RECENT

Sunday, September 25, 2016

Jicho La 3: Kichuya si wing mzuri, Mwashuiya si mchezaji wa benchi Yanga, tatizo Ferguson, Simkoko, wameondoka na ‘uchawi’ wote…

????????????????????????????????????
Na Baraka Mbolembole
STEVEN Mapunda ‘Garrincha’ na Said Maulid ‘SMG’ ni wings wa kwanza wa ‘kizazi cha miaka ya 2000’ ambao walitikisa sana Tanzania kutokana na uchezaji wao wa kasi wakitokea upande wa kulia mwa uwanja. Ma-wings hawa wanabaki kuwa bora kihistoria kwa maana tayari wameshastaafu soka la ushindani.
Mapunda na SMG ni kati ya wachezaji wa kizazi kipya ambao walikuwa wakicheza kizamani-kwa maana ya kubaki tu sehemu ya pembeni ya uwanja na kutegemea kukimbia na mpira au kukimbia pasi iliyo ‘njiani.’
Wakati fulani, Saimon Msuva alionekana kama anaweza kuwa ‘Steven Mapunda mpya’ lakini mifumo ya uchezaji imemzua, huku pia akiwa si mpigani mzuri wa krosi. Sifa nyingine muhumu ambayo iliwafanya Garrincha na SMG kutamba ni upigaji wa krosi timilifu ambazo zilifika kwa walengwa.
Pengine ‘uhaba’ wa washambulibji wenye uwezo wa kucheza mipira ya juu ndio umechangia kwa kiasi kikubwa kumepunguza ma-wing wenye ‘krosi bomba,’ ama inawezekana mbinu za makocha wa kisasa, mifumo ya kiuchezaji ama ni kupungua kwa wachezaji namba 7 au 11 wenye maarifa binafsi yenye kuzalisha magoli mengi kwa timu yake.
Hakika hiki si kizazi cha David Beckham wala Sergio Conceicao, hizi si nyakati za wakufunzi kama John Simkoko ndiyo maana wachezaji kama Paul Pogba na makocha kama Mexime wanatawala.
Kama ningekuwa kocha ningependelea mfumo wa 4-4-2 ambao ni rahisi kwa wachezaji wa England ama hapa Tanzania.
Mfumo huu usingempa, Msuva tuzo binafsi za ufungaji bora na mchezaji bora wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa 2014/15, lakini unaweza kumpa magoli zaidi ya 30 Zlatan Ibrahimovic pale England. Licha kuwa ni kibabu, Ibrahimovic angefunga kwa ustadi mkubwa magoli matatu katika krosi tano za David Beckham.
Rooney alifunga magoli 27 katika EPL msimu wa 2009/10 huku ustadi wake kuruka juu na kufunga kwa kichwa ukichagizwa na krosi maridadi na timilifu kutoka kwa Antonio Valencia.
Si Alex Ferguson hakuwa na vikosi vikali lakini alikuwa na ‘mbinu za kichawi.’ 4-4-2 imempatia heshima ya miaka yote katika soka la Kingereza kama ambavyo makocha wengi wanavyoangaika kuvunja rekodi ya Simkoko pale Mtibwa Sugar.
Nisingependelea kabisa kuichezesha timu yoyote ya Tanzania mfumo wa 4-3-3, na kama ningekuwa mshauri wa Jose Mourinho ningemshauri aachane na mbinu zote na kwa kuwa nafahamu ubora wake wa kimbinu ningemwambia ‘a-copy na ku-paste’ 4-4-2 ya Sir Alex. Rooney ni namba 10 bora zaidi England na Valencia si namba 2 na wing bora zaidi wa kulia pale England.
Unawakumbuka, Abuu Mkangwa, Geofrey Mhando, Moja Liseki, Abdallah Juma-Mzanzibar pekee kushinda tuzo ya ufungaji bora VPL. Hao niliokutajia hapo wote wamefanya mambo makubwa pale Mtibwa na wameshinda tuzo za ufungaji bora VPL wakiwa pale.

Hii ni kuhusu Serikali ya Kenya kukuzawadia Dola Elfu Ishirini….Endapo tu!!

Taarifa hii ikufikie mtu wangu wa nguvu kutoka Afrika Mashariki. Mamlaka nchini Kenya imetangaza zawadi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa taarifa zozote zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ugaidi anayetafutwa kwa tuhuma za kupanga shambulizi katika mji wa pwani wa Lamu.
Bundle of dollars banknotes on 100 dollars background
Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya imesema, mtuhumiwa huyo, Ramadhani Kioko, anadaiwa kuhusika na shambulizi la kigaidi lililotokea Lamu ambapo askari watano wa jeshi Kenya walijeruhiwa baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa kando ya barabara Julai 26 mwaka huu. Wizara hiyo pia imesambaza picha za mtuhumiwa huyo ambaye wanaamini kuwa alitega bomu hilo katika eneo la Ishakani, mashariki mwa mji wa Lamu.
Hatua hiyo imekuja baada ya wizara hiyo kutangaza zawadi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa mtu yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa mwingine wa ugaidi Abdullahi Abdi Sheikh, ambaye anadaiwa kupanga mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi ikiwemo shambulizi lililoshindwa dhidi ya kambi ya jeshi ya Baure kwenye kaunti ya Lamu.